Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 23910 articles
Browse latest View live

MKALI NUH MZIWANDA ASEMA KURUDIANA NA SHILOLE NI KITU CHA FEDHE KWANGUA

$
0
0
Msanii Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Alikiba amefunguka na kusema kuwa hata kama ikitokea mpenzi wake huyo wa zamani akitaka kurudiana na yeye ni kitu kisichowezekana kwa sasa.

Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana Nuh Mziwanda amesema kuwa kwa sasa yeye amefunga ukurasa wa mapenzi na Shilole hivyo hata ikitokea akataka kurudiana na yeye hawezi kufanya hivyo kwani ameshaanza maisha mapya ambayo anaona ni ya furaha zaidi.
Mbali na hilo Nuh Mziwanda ameeleza kuwa kwa sasa hataki tena maisha ya kiki na skendo alizoita kuwa ni za ajabu ajabu bali anataka kujenga jina lake kutokana na kazi zake kwenye muziki pamoja na kutengeneza muziki kama 'Producer'

TAZAM PICHA ZA MILLEN MAGESE ALIVYO KUWA ANAKULA BATA KWENYE HOTEL YA HYATT

$
0
0
Elephant-Man
Miss Tanzania mwaka 2001 na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese ametupia picha kwenye akaunti yake ya Instagram ambazo zimeonekana kuwadatisha njemba wengi.

Millen kwa sasa yupo kwenye kampeni kubwa ya kutafuta tiba ya ugonjwa wa Endometriosis unaomsumbua kwa miaka 13 mpaka sasa lakini haujamzuia kuonesha urembo wake.
160504102420_instagram_512x288_bbc_nocredit
Mwanamitindo huyo ambaye anafanya kazi zake nchini Afrika Kusini kwa sasa yupo nchini Tanzania kwa ajili ya mapumziko na shughuli zake binafsi amepost picha kwenye Instagram na kuandika: Tuwe na utamaduni wa kupenda vya kwetu na kusifia vya kwetu . Na kutangaza vya kwetu……Tanzania is beautiful ….. Tutembelee vya kwetu . #SmallVacayInTanzania🇹🇿HyattHotel . Next……Wish to go to Serengeti and Saadani #TakingTimeOff.”
Tazama picha zaidi:
33C6F7BE00000578-3570857-Ranieri_holds_a_blue_boot_with_the_words_Champions_2015_16_on_it-a-41_1462268693651
10422134_812063695567669_5972704573303766519_n
Tambwe-Ngoma-1-e1443282353514

CHANZO na Bongo5.

KESI YA ELIZABETH MICHAEL LULU MPAKA 2017

$
0
0


Kesi ya staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ya kudaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba huenda ikaanza kusikilizwa mwakani (2017), Amani limeambiwa.


 Kwa mujibu wa chanzo kilichopo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inayosikiliza keshi hiyo, japo wananchi wengi wamekuwa wakisubiri siku ya kesi hiyo kusomwa lakini ukweli ni kwamba hakuna dalili yoyote ya kuanza kusikilizwa mwaka huu kwa vile mahakama hiyo ina kesi za watuhumiwa walioko mahabusu hivyo kuwamaliza kwanza hao. “Kesi ya Lulu kwa mwaka huu msahau kabisa. Hii kesi kutajwa labda kuanzia mwakani maana hakuna dalili yoyote na haipo kwenye listi ya kesi za mwaka huu. 
 
“Wale ambao walikuwa na shauku ya kujua kitakachojiri, hayo mambo ni mwakani maana mpaka sasa kesi ambazo zinapewa kipaumbele ni za watuhumiwa ambao wapo mahabusu magerezani.  “Ujue kuna kesi nyingi ambazo hazijasikilizwa.

 Kwa hiyo hizo ndo’ zinapewa nafasi ya kwanza kuliko kesi kama ya Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana,” kilisema chanzo hicho. Ili kujiridhisha, gazeti hili lilimtafuta wakili wa msanii huyo, Peter Kibatala ambaye alijibu kwa kifupi: “Binafsi sifahamu kuhusiana na hilo, mpaka sasa sijajua hiyo kesi itakuwa lini kwa sababu sijaona ikipangiwa siku.”

LIVERPOOL YATINGA FAINALI EUROPA CUP, YAITWANGA VILLARREAL

$
0
0




Liverpool: Mignolet, Clyne, Toure, Lovren, Moreno, Can, Lallana, Milner, Coutinho (Allen 83 mins), Sturridge (Lucas 92), Firmino (Benteke 90) 
Subs not used: Ward, Ibe, Skrtel, Smith
Booked: Clyne 
Goal: Soriano (og) 7, Sturridge 63, Lallana 81
Villarreal: Areola, Mario, Musacchio, Victor Ruiz, Jaume, Jonathan (Bonera 73), Pina (Trigueros 60), Bruno, Suarez, Soldado (Adrian 69), Bakambu 
Booked: Victor Ruiz, Soldado, Suarez
Sent off: Victor Ruiz 
Subs not used: Sergio Asenjo, Samuel, Castillejo, Rukavina
Referee: Viktor Kassai (Hungary)





SUPER STAR WEMA SEPETU APAGAWISHA TENA ,AJITOKEZA HADHARANI,UMBO LAKE LA SASA LAIBUA MAZITO MAPYA ZAIDI TEAM WEMA WAIBUKA NA HILI

MASTAA WEMA SEPETU GIGY MONEY VITA KALI YA KUMGOMBEA IDRISS,GIGY ATAMBA KUMCHUKUA MCHANA KWEUPE,TEAM WEMA WAMSHUKIA VIKALI

$
0
0

Juzikati lilifanyika bonge la pati pale Regency Hotel, Mikocheni jijini Dar lililokwenda kwa jina la Pool Party ambapo mbali na matukio mengine, msanii
Gift Stanford ‘Gigy’ na mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, Idris Sultan walisababisha gumzo baada ya kugandana kisha baadaye kudaiwa kuondoka pamoja.  

SUPER STAR WASTARA AGOMA KUOLEWA NA KIJANA,AFUNGUKA MAZITO

$
0
0
Mahari yaliyotolewa wiki mbili zilizopita kwa staa wa filamu Bongo, Wastara Juma, yamerudishwa kwa mwanaume aliyetaka kumposa, Juma Mbega, kwa kile kilichodaiwa kuwa msanii huyo amepinga vikali kuolewa na kijana huyo ambaye naye ni mwigizaji wa sinema za Kibongo. Wiki mbili zilizopita Mbega alimtuma mshenga wake, Hamis Ramadhan kwenda kwa akina Wastara
kupeleka mahari ya shilingi milioni tano, akitaka kumuoa staa huyo baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na Mbunge wa Donge kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sadifa Juma. Akizungumza kwa uchungu, Mbega alisema kuwa aliumia kupokea habari mbaya kutoka kwa mshenga wake huyo kwamba mwanamama huyo aliyarudisha mahari hayo na kwamba hataki kuolewa kwa sasa.

 “Namjua Wastara vilivyo, nilitamani sana mwanamke kama yeye kwa kuwa najua wengine hawawezi kuishi naye kwa upendo zaidi ya aliyekuwa mtu wangu wa karibu, marehemu Sajuki (Juma Kilowoko) na mimi mwenyewe,” alisema Mbega aliyekuwa rafiki mkubwa wa Sajuki. Mbega alisema kuwa, pamoja na kurudishiwa mahari, lakini bado hajakata tamaa ya kumfukuzia Wastara kwani anaamini ndiye mwanamke wa maisha yake. 


“Sijakata tamaa, naamini ipo siku atakubali, najua wazi hakuna mtu atakayemfaa zaidi yangu,” alisema jamaa huyo. Kwa upande wake Wastara, alisema aliyarudisha mahari kwa kuwa Juma ni kama mdogo wake aliyemlea hivyo asingeweza hata siku moja kukubali kuolewa naye. “Jamani yule nimeona ni kama mdogo wangu ndiyo maana nimerudisha mahari yake na siwezi kuolewa naye,” alisema Wastara. Kabla ya kuibuka kwa Mbega, Wastara alivurugana na Sadifa ambapo kila mmoja alichukua hamsini zake.

CREDIT; GPL

PETE YA UCHUMBA YA SUPER STAR LULU YAZUA GUMZO SIRI NZITO YAFICHUKA

$
0
0





Elizabeth Michael ‘Lulu’ akionyesha pete yake ya uchumba. MSANII maarufu wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibua gumzo kubwa baada ya hivi karibuni kutinga kwenye Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar akiwa ametinga pete ya uchumba.


Lulu akiwa ametinga kigauni chake kifupi cheupe alifikia kwenye ‘red carpet’ na kuanza kupigwa mapicha huku akiweka mapozi tofauti lakini kila pozi alilokaa alihakikisha pete hiyo inaonekana. “Hee, huyu Lulu kavishwa lini hii pete, na nani? Au ndiyo yule bosi wa redio?” alisikika akihoji mmoja wa wadada waliokuwa eneo hilo na kuwafanya wengine waanze kumjadili. Ndani ya ukumbi huo ilikuwa vigumu kuongea naye na alipopigiwa simu ili azungumzie undani wa pete hiyo hakupokea

MBUNGE WA CHADEMA ATOLEWA BUNGENI NA ASKARI CHINI YA ULINZI MKALI

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson leo amewaamuru askari wa Bunge kumtoa Bungeni Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara baada ya mbunge huyo kutaka kumfanyia fujo mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma Holle wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria

URAIS WA CONGO WAMPONZA KATUMBI, JESHI LA DR CONGO LAMZIGIRA KWAKE, TAARIFA ZAELEZA NI FIGISU ZA RAIS KABILA

$
0
0
Takribani saa 14 tu baada ya mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe kutangaza nia yake ya kuwania Urais wa DR Congo, askari wa jeshi la nchi hiyo wameizunguka nyumba yake anayoishi.
TP Mazembe ndiyo timu aliyochezea Mtanzania, Mbwana Samatta na kupata jina kubwa kabla ya kujiunga na KRC Genk ya Ubeligiji. Lakini bado Mtanzania, Thomas Ulimwengu anaendelea kuichezea timu hiyo.
Taarifa zimeeleza, Serikali ya DR Congo imetoa kigali cha kukamatwa kwa Katumbi kwa maelezo kwamba amekuwa akikiuka mambo kadhaa na tayari wizara ya ulinzi ya DR Congo imesema inataka afunguliwe mashitaka.
Hata hivyo kumekuwa na taarifa za kutaka kumbana Katumbi ikielezwa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambacho ni kirefu cha DR Congo anaonekana kutofurahishwa na hilo.
Katumbi ambaye anaaminika kwa sasa ndiye Mkongo maarufu kuliko wote duniani, amekuwa presha kubwa kwa Rais Kabila.
Bado haijaelezwa mwisho wa askari hao wa DR Congo, lakini taarifa nyingine zimesema Katumbi analindwa na askari kutoka Marekani na Afrika Kusini ambao wana mafunzo ya juu kabisa.

KATIBU MKUU CHADEMA JIPUUU

$
0
0
By:Nasri Bakari BossNgasa Official Website
Kiukweli huyu katibu mkuu hajui hata pa kuanzia Chama kinaonesha dalili za kuifuata TLP na UDP sioni harakati zake ki ukweli CHADEMA ilikosea sana Dr. Mashinji ni unpopular figure hata akitembea kwa miguu Karikoo hakuna wa kumshitukia kuwa ni kiongozi.
Ukimya wake ni hatari kwa mustakabari wa chama kwani watu wasiokuwa na vyeo kama akina Lowassa ndo wamekuwa msaada mkubwa kukisemea chama kwa sasa. Anaonekana kabisa ni uteuzi ambao ulikosewa na ni mtu asiyekua na ushawishi ndani ya chama.
Kutoka kwenye nchi ya viwanda mpaka nchi ya majipu alikuwa ana mengi ya kuongea lakini yupo kimyaa wakisubiri kuzungusha mikono mwaka 2020.
Huku serikali ya Magufuli ikijisafishia njia inaonekana haitapata upinzani mwaka 2020 kutokana na uchakavu wa CHADEMA.

BILIONI 6 ZA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KUNUNULIA MADAWATI ZAIBUA MAJIPU JESHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood, Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, akidai kutapeliwa na maofisa wa jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), katika utengenezaji wa madawati ya bei nafuu kama Rais Dk. John Magufuli alivyoagiza.
Maduhu akiwaonesha waandishi wa habari picha mbalimbali walizopiga na maofisa wa majeshi hayo walipofika kufanya kikao na uongozi wa kiwanda hicho.
Maduhu akionesha madawati yanayotengenezwa na kiwanda chake.
Moja ya mashine zinazotumika kutengeneza samani mbalimbali katika kiwanda hicho.


Na Dotto Mwaibale


SHILINGI bilioni 6 zizotengwa na Rais Dk.John Magufuli kwa ajili ya utengenezaji wa madawati zimeibua majipu katika Jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), kwa kudaiwa kumtapeli Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood, Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu katika utengenezaji wa madawati.


Maduhu amezilalamikia taasisi hizo za jeshi akidai zimemtapeli katika kazi ya kutengeneza madawati hayo baada ya kukubaliana kufanya ushirikiano wa kazi hiyo kufuatia wao kuelemewa.


Maduhu alitoa lawama hizo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutapelewa na majeshi hayo waliofika kiwandani kwake kuomba ubia wa kushirikiana kutengeneza madawati ya bei nafuu kama alivyoagiza Rais.


Hata hivyo, Mkuu wa Kiwanda cha Magereza, ACP Ismail Mlawa, alisema baada ya serikali kutoa ‘order ya kutengeneza madawati hao, taasisi hizo mbili ziliunda timu maalumu ya kutengeneza madawati hayo.


Alisema, baada ya kuunda timu hiyo, walikubaliana kuzunguka kwenye viwanda mbalimbali nchini kwa ajili ya kuangalia vifaa na sampuli ya utengenezaji wa madawati hayo ili yaweze kuwa katika ubora unaokubalika.


Alisema, kutokana na hali hiyo, timu hiyo ilikwenda kwenye viwanda mbalimbali kikiwamo hicho cha Edosama kwa lengo la kuangalia upatikanaji wa vifaa na si vinginevyo.


“Tulienda kwenye viwanda zaidi ya vinne kikiwamo cha Edosama, lengo ni kuangalia namna ya upatikanaji wa ‘material’ (vifaa) vya kutengeneza madawati pamoja na kufanya ‘window shoping’ lakini katika viwanda vyote hivyo, hakuna hata kimoja tulichoingia nacho mkataba wa kutengeneza madawati kwa sababu hatukuwa na mamlaka ya kufanya hivyo mpaka tutakapowasilisha taarifa kwa viongozi wetu,”alisema Mlawa.


Aliongeza, baada ya kuona wanavyotengeneza madawati hao, walilazimika kuwasilisha taarifa hiyo kwa viongozi wao ili waweze kujadiliana kuhusiana na suala la utengenezaji wa madawati hao.


Maduhu alisema Aprili 12 mwaka huu walipigiwa simu na maofisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza ambao walifika katika kiwanda chao na kufanyanao vikao vinne kuanzia Aprili 12 na 15 mwaka huu.


Alisema maofisa wa majeshi hayo walioshiriki vikao hivyo ni Kanali Wanyancha na Tendwa Mahunnah wote kutoka JKT na ASP Mlawa pamoja na ofisa mwingine wa Jeshi la Magereza ambaye jina lake halikupatikana.


Maduhu alisema kwamba katika kikao hicho jumla walikuwa saba pamoja na maofisa wa kiwanda hicho na kuwa katika kikao hicho walifanikiwa kupiga picha za mnato, kurekodi mazungumzo yote.


Aliongeza kuwa katika kikao hicho maofisa hao wa jeshi waliwaeleza kuwa wamefika kiwandani hapo baada ya kushindwa bei ya madawati iliyotolewa na Rais ya sh.50,000 kwa kila dawati kwani gharama zao za kutengeneza dawati moja ni zaidi ya sh.78,000.


Alisema kwamba katika kikao hicho walikubaliana kiwanda hicho kipewe kazi ya kusambaza vyuma vya miguu ya madawati hayo vyenye ukubwa wa inchi 1x1-1.5 mm vikiwa vimepakwa rangi.


Maduhu alisema baada ya kukubaliana walianza kuwapa teknojia ya utengenezaji wa madawati hayo huku wakiendelea kuandika hadi waliporidhika na gharama ya kutengeneza dawati moja kwa sh.38,000 na sh.40,000 kwa teknolojia ya kiwanda hicho.


Alisema baada ya kupata teknolojia hiyo walikata mawasiliano na kila walipokuwa wakiwapigia simu walikuwa hawapokei.


Alisema kiwanda hicho kimetumia zaidi ya sh.bilioni moja kwa ajili ya utafiti wa miaka mitano kwa kutembea viwanda katika nchi 17 ili kujifunza teknolojia hiyo na kuwa wao wamekuwa wa kwanza kubuni aina mpya za madawati hapa nchini.

THE MAGAZETI YA BONGO LEO FRIDAY/IJUMAA 6/5/2016 LIVE!!

HUU NDIO UJUMBE WA DIAMOND ALIYOMWANDIKIA ZARI KATIKA SIKU YA MAMA DUNIANI

$
0
0


Ujumbe wa Diamond kwa zari (mothers day)

From @diamondplatnumz - A very Special Mother's day to this Beautiful and Humble soul of Mine @zarithebosslady ... i wish you can understand how much i love you, Mpaka natiwa Dripu😥....wenyewe wanasema kuzaa sio tija, ila kumpata Mwanamke akajua kumlea mtoto wako Vyema ndio kazi inakuwaga hapo... Shukran sana kwa zawadi hii kubwa ya Mtoto mzuri na kuendelea kumlea vizuri..... sjui na lile jipu pia Ntumbue😃.... aaagh! Anyway'z😝🙋 tutakutana Mbeleni

GIGY MONEY MATONYA KUNA KITU,WANASWA WAKIWA KWENYE POZI TATA

$
0
0
Video queen asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stamford ‘Gigy Money’ akiwa katika pozi na mbongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’.
Habari zilizoenea wikiendi iliyopita zilidai kwamba, kuna kitu kinaendelea kati ya video queen asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stamford ‘Gigy Money’ na lejendi wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’ kufuatia kusambaa kwa picha zao kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha wakiwa  kwenye mahaba mazito.

 Kwa mujibu wa watu wa karibu wa wawili hao, kuna
uwezekano mkubwa Matonya akawa ndiyo amefika kimapenzi kwa Gigy lakini wapo wanaosema mwanadada huyo anatafuta kiki. Wikienda lilimsaka Matonya ili afungukie kinachoendelea lakini alipokosekana hewani, alitafutwa Gigy ambapo alifunguka
Gigy, Matonya kuna kitu!
juu ya ishu hiyo: “Hizo ni picha tu, kama watu wanataka kumjua shemeji yao wasiwe na haraka kwani watamuona ‘soon’




WAZIRI AUNDA KUNDI LA KUMPINGA MAGUFULI 2020,UMAFIA WA KUKWAMISHA BAJETI WANASWA

SAKATA LA SUKARI VIGOGO WANBANWA KILA KONA

BREAKING NEWS: SAKATA LA SUKARI MBUNGE WA CCM ATAJWA

MAMA WA SUPER STAR SNURA AANGUKA GHAFLA,NI BAADA YA CHURA KUFUNGIWA

$
0
0

 
Wakati Wabongo wakiwa wamecharuka mitandaoni kuuzungumzia wimbo wa Chura wa Snura Mushi, nyuma ya mijadala hiyo, kuna habari ya kuhuzunisha, mama mzazi wa msanii huyo, Doto Sanzegara, alijikuta akianguka kwa mshtuko baada ya serikali kutangaza kumzuia mwanaye huyo kujihusisha na kazi za sanaa, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi. 



ALIZUIWA NA BASATA 
Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) walitoa tamko la wimbo huo kutopigwa katika vituo vya redio na televisheni nchini pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kwa kile walichoeleza kuwa umekiuka maadili hivyo pia kumfungia kazi zake mpaka pale atakapojisajili katika chombo hicho kwa kuwa licha ya kufanya kazi za sanaa kwa muda mrefu, msanii huyo hakuwa amejisajili. 
HABARI KAMILI
 Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia, wakati serikali inatoa tamko la kumsimamisha Snura, Mei 4, mwaka huu, mama huyo alipata taarifa kupitia redio, ndipo alipopata mshtuko, akaanguka na kupoteza fahamu. “Yaani ile anasikia tu redio inatangaza, mama alikuwa amekaa kibarazani, akaanguka palepale ghafla. Ikawa mshikemshike kunusuru uhai wake. Ikabidi ndugu waliokuwa pale nyumbani waanze kumpa huduma ya kwanza kwa kumpepea. 
APEPEWA
 “Walianza kumpepea pale nyumbani huku wengine wakitafuta usafiri wa kumpeleka Mwananyamala Hospitali, lakini bahati nzuri kabla hawajapata  gari, mama alizinduka na kurejea katika hali ya kawaida.
 WAMPA UANGALIZI MZITO 
“Ilibidi baadhi ya ndugu ambao walikuwa mbali wasogee nyumbani kwa ajili ya kumwangalia afya yake kwa ukaribu zaidi,” kilisema chanzo hicho.
MAMA ANA TATIZO HILO
 Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kuwa, mama Snura huwa ana tatizo hilo hususan pale anapopata habari ya mshtuko na kwa sababu Snura alikuwa miongoni mwa watoto ambao amekuwa akiwategemea, habari za kufungiwa zilimshtua sana. “Bi mkubwa aliona ni janga maana Snura ndiyo kila kitu kwake. Anajitoa sana kumsaidia mama yake hivyo kitendo cha kufungiwa sanaa, kilimpa tafsiri ya haraka kuwa pengine watakufa njaa,” kilisema chanzo hicho. 
APEWA HABARI NJEMA 
Baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida, mama Snura alipewa taarifa kuwa mwanaye huyo ameshakamilisha taratibu zote zilizotakiwa na Basata hivyo yupo huru kuendelea na sanaa lakini kwa angalizo la kuufanya upya wimbo wa Chura kwa kutoa
sehemu ambazo zimekiuka maadili.

 
 NDUGU WAMYOSHEA KIDOLE SNURA 
Mjomba wa Snura ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa kutokana na tukio hilo, wamemuonya msanii huyo kuwa makini na kazi zake za sanaa ili zisiweze kumsababishia matatizo mzazi wao. “Tumemuonya maana katika hili hana sababu ya kujitetea. Yeye ndiye sababu ya mama yake kuanguka. Tumemwambia awe makini maana asingetoa Chura ambayo imekiuka maadili wala hiyo serikali isingetamka kuwa inamfungia,” alisema mjomba huyo.
 SNURA HUYU HAPA
 Baada ya kuzinyaka habari hizo, Jumamosi iliyopita, mwanahabari wetu alimvutia waya Snura ambaye alikuwa safarini kuelekea jijini Mwanza ambapo alipopokea alikiri kumsababishia mshtuko huo mzazi wake, lakini akasema anamshukuru Mungu suala hilo limepita salama. “Wee ilikuwa mbaya sana lakini namshukuru Mungu limepita salama. Mama yuko poa, mimi naendelea na mizunguko ya kazi zangu za sanaa, Chura anakuja kivingine hivyo mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Snura.
 KUMBUKUKUMBU 
Kabla ya kutoa wimbo wa Chura, Snura ametoa nyimbo kadhaa zilizotamba mjini ikiwemo Majanga ambayo bado inaendelea kufanya vizuri katika anga la muziki.
 MUHIMU Baada ya kukamilisha taratibu zote Basata na kuwa huru, Snura alizungumza na Global TV online, mahojiano yake yatarushwa hivi karibuni kupitia www.globaltvtz.com 

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

MZEE WA MIAKA 124 ATOA SIRI YA KUISHI MIAKA MINGI.

$
0
0
MTU aliyeshiriki Mapinduzi ya Zanzibar akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, Machano Mjomba Machano amezungumza na gazeti hili kuhusu siri ya umri wake na alivyoshiriki kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika 1964.
Mzee huyu ambaye familia yake inamkadiria kuwa na umri wa zaidi ya miaka 124, anaishi Gamba Mabatini, kilometa 25 kutoka Bandari ya Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Machano ambaye anamshukuru Mungu kwa umri alionao, alisema alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika kumlinda Rais Sheikh Abeid Amani Karume wakati alipotangaza mapinduzi hayo redioni , eneo la Rahaleo.
Pamoja na masuala mengine, alisema walifanikisha mapinduzi hayo kutokana na kushikamana na kuwa na usiri mkubwa. Aidha alisema kwamba John Okello; aliyekuwa raia wa Uganda, alitumika kuwapa mafunzo ya kazi.
Mzee Machano ambaye ameona vizazi vingi vilivyokuja na kupita, inaelezwa kuwa hakuna mtu anayejua umri wake kwa usahihi. Hata yeye anasema aliambiwa umri wake wa takribani miaka 70, wakati wa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Mtoto wake wa pili kuzaliwa kutoka mwisho, Musa Machano Mjomba ambaye ni mwalimu, alisema wanamkadiria baba yao kuwa na umri wa zaidi miaka 124. Mtoto wake wa nne kuzaliwa kati ya watoto 13 aliojaliwa, ana umri wa miaka 80 .
Ni nini sifa ya kuishi na kuona uzee mwema kama maandiko matakatifu yanavyosema? Soma makala ukurasa wa 15, Mzee Machano akieleza siri ya umri wake na nafasi yake katika Mapinduzi ya Zanzibar.
Viewing all 23910 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>