Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 23910

EFM YAMBURUZA MTANGAZAJI PAUL JAMES MAHAKAMANI

$
0
0
picha-ya-pj
Mtangazaji wa Clouds FM, Paul James aka PJ ameshtakiwa mahakamani na kituo cha redio cha EFM kwa kuvunja mkataba kinyemela.

Mtangazaji huyo aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi huu na kurejea kwenye kituo chake cha zamani, Clouds FM, alichoondoka pamoja na mwenzake Gerald Hando. EFM imefungua mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.
Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya shilingi milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
efm-radio-page-001
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam

Viewing all articles
Browse latest Browse all 23910

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>