Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 23910

JOH MAKINI ATOA FURSA HII KWA WADADA KUJIUNGA WEUSI

$
0
0
Rapa Joh Makini ambaye anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Perfect Combo’ amefunguka na kusema kuwa milango iko wazi kwa wasanii wa kike kujiunga na kundi la Weusi na kufanya nao kazi.

Joh Makini amesema hayo jana kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho kilikuwa kinaruka moja kwa moja kutokea Kituo cha Mabasi cha Sinza Jijini Dar es Salaam ‘Simu 2000’ ambapo moja ya shabiki wa kike aliomba nafasi kujiunga na kundi hilo pindi atakapo maliza shule.
johmakinitz-20161025-0002
Weusi
“Milango iko wazi kwa wadada kuja kuungana nasi, na tuombe Mungu kwani muda si mrefu tunampango wa kuja na ‘Label’ ya Weusi ambayo itatoa nafasi kwa wasanii mbalimbali” alisema Joh Makini
Mbali na hilo Joh Makini alifafanua kuwa toka ameanza muziki hajawahi kuwa na tofauti na mwanamuziki yeyote yule kwani yeye hafikiri kuwa na tofauti na msanii mwingine kama itamuongezea kitu
“Toka nimeanza muziki sijawahi kuwa na bifu na mtu yoyote, sijawahi kufikiri kuwa na tofauti na mtu inaweza kuniongezea kitu, mimi na ‘deal’ na muziki wangu” alisema Joh Makini

Viewing all articles
Browse latest Browse all 23910

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>