Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 23910 articles
Browse latest View live

BENKI YA UBL YAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KILIMO NCHINI TANZANIA

$
0
0
Benki ya UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na Serikali yake. 

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Bw. Jamall alisema kuwa kwa sasa Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala la ukuaji wa uchumi ingawa kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa fedha zimeadimika mitaani lakini ni wazi kwamba Taifa linarudi kwenye utaratibu. Hivyo wameonesha nia ya kuwekeza hasa katika Sekta ya Kilimo.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa hali inabadilika na Jumuiya ya Mabenki inaanza kuwa na imani na Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha Benki ya UBL kuonesha nia ya kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni jambo jema katika maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa Sekta hii mama bado inakabiliwa na changamoto nyingi.  

Alisema dhamira kubwa ya Benki ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja na uvuvi. Na Serikali imeahidi kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze kupiga hatua ya haraka zaidi hasa katika kipindi ambacho imedhamiria kuwa nchi ya Viwanda.

Akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya dola katika uchumi badala ya shilingi ya Tanzania, hasa kwenye mikopo, Waziri Mpango alisema kuwa suala hili Serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa karibu biashara ya maduka ya fedha za kigeni. 

“Tumepiga hatua ya kufunga mashine za kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuona kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe kodi inayostahili. Aidha zoezi hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania – BoT, kuona kiasi cha fedha za kigeni zilizopita katika maduka na itaimarisha matumizi ya shilingi ya Tanzania; japo tuna changamoto kubwa ya wananchi kutokudai risiti pindi wanapopata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni,” Alisisitiza Dkt. Mpango.

Katika kuhitimisha majadiliano hayo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mpango alisema Serikali itaongeza ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa Benki hiyo ni miongoni mwa Benki kubwa katika nchi za Uarabuni.

Imetolewa na: 
Kitengo na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
16 Februari, 2017
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya Kielektroniki (EFDs) yalivyoongeza Makusanyo ya Mapato ya Serikali alipotembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), Ofsini kwake jijini Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya kutaka kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya Mtendaji huyo kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza nia ya kuzitumia fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada ya kukutana na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall OfIsini kwake jijini Dr es salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

ANGALIA HAPA PICHA ZA SHOW YA STAA MARIAH CAREY HUKO MAREKANI

TAZAMA PICHA MPYA YA STAA JENNIER LOPEZ

DADA WA DIAMOND PLATNUMZ ALIA KUKOSA WANAUME

$
0
0

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri akiwa chini ya Lebo ya ‘WCB’, ‘Queen Darleen’ amefunguka kuwa anaumizwa sana na hali ya kuishi bila mpenzi jambo ambalo limekuwa likimuumiza sana katika maisha yake ya sasa maana yeye pia anahitaji kupenda na kupendwa kama walivyo watu wengine.

Akichonga na Showbiz Xtra, Queen Darleen alisema kuwa, tangu aachane na mzazi mwenziye aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike hajawahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi jambo ambalo amekuwa akijiuliza bila kupata jibu kuwa linasababishwa na nini.

“Naumizwa na hii hali, kuna wakati huwa nafikiria wanaume wananiogopa au sijui ni kitu gani kinatokea sasa nahitaji kuwa na mpenzi,” alisema Darleen.

RAPA NAY WA MITEGO ADAI ANA LIST YA WASANII WANAOBEBWA HAPA BONGO

$
0
0

Imekua desturi ya Nay wa Mitego kuandika mistari ya utata kwenye baadhi ya ngoma zake,kitu ambacho kimejitokeza tena pia kwenye wimbo wake mpya, Muda Wetu.

Kwenye ngoma hiyo, Nay amedai kuwa kuna wasanii ambao wanabebwa kwa kupewa promo kubwa lakini promo ikikata wanabaki hawana lolote. Kwenye mahojiano na kipindi cha Supermega kupitia Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove, Nay ameweka wazi kuwa anafahamu wasanii hao na yupo tayari kuwaweka hadharani.

““Nafikiri hiyo tuwape kazi wananchi watuorodheshee ni msanii gani kwa kipindi hichi anaishi kwa upepo wa promotion na upepo ukikata tutaona reaction zake,” amesema Nay.

Amedai kuwa yeye baada ya kupata matokeo makubwa ya ngoma hiyo,ataweka wazi list ya wasanii ambao anaamini kwa asilimia zote kuwa wanabebwa na washkaji zao ambao wapo kweny

RAPA NAY WA MITEGO AFUNGUKA MENGINE TENA KUHUSU MR.T TOUCHEZ

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop bongo Emmanuel Elibariki a.k.a 'Nay wa Mitego' amesema hawezi kushuka kimuziki kwa kuachana na producer Mr. T Touchez na kusema kuwa hajawahi kuanguka katika muziki wake kutokana na maneno  ya watu wanaomuombea mabaya.

Amefunguka hayo wakati akijibu maswali ya watu katika kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV ambapo kuwa walitoa maoni yao kuwa ameshuka kimuziki baada ya kuachana na aliyekuwa producer wake Mr. T Touchez.
Amesema kuwa hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kubadilisha upepo wa muziki wake na kwamba yeye anamuamini Mungu wake ambaye anapatia riziki, na kuongeza kuwa hashangazwi na maneno hayo kwa kuwa huwa hana bahati ya kusemwa kwa mazuri pindi anapokuwa karibu na mtu na baadaye kuachana naye, iwe kimapenzi au kikazi.
"Siwezi kushuka kwa ajili ya maneno ya watu na mimi na kwa sababu mimi ninamuamini Mungu wa dunia yangu ambaye kila nikimuomba ananijibu kwa wakati. Pia mimi siyo msanii aliyedumaa hivyo hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kubadilisha upepo wa muziki wangu. Si mnaona sijiwezi inakamata Top 10 vituo mbalimbali hivyo sijashuka kimuziki". Alisema Nay wa Mitego
Nay wa Mitego akiwa KIKAANGONI
Nay ameongeza kuwa katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi na Mr. T Touchez alikuwa akimthamini kama producer ambaye anastahili kufanya kazi katika mazingira mazuri ndiyo maana hata kazi nyingine zilizokuwa zikifanyika katika studio yake ya Free Nation hakuwahi kumdai pesa yoyote ya kazi hizo.
 Aidha Nay ameeleza kuwa hana kinyongo na producer wake huyo ambaye walikwaruzana zaidi ya miezi sita iliyopita huku akiwa amegoma kueleza chanzo cha ugomvi wao na producer huyo aliyemuandalia 'hits' kadhaa.
"Sina kinyongo na Mr.T Touchez hata kidogo nipo tayari kufanya naye kazi kama akisema kwa sababu siwezi kuishi kwa kulipiziana visasi, na wala siwezi kujibizana naye, maana baba hawezi kujibiana na mtoto" alisema Nay.

MSANII BARNABA AMPIGIA MAGOTI ICE BOY LAIVU

$
0
0
Msanii wa bongo fleva Barnaba amemuomba msamaha Ice Boy kwa kumcheleweshea mafanikio katika  muziki wake, kama Ice Boy mwenyewe alivyowahi kudai.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Barnaba amesema  "Naomba tena radhi kwa jamii kwa kauli ya Ice aliyosema kwamba mimi ndiye nimemchelewesha kufanikiwa katika muziki wake kwa kuwa sipendi kugombana na kukwanzana na mtu namuomba radhi kupitia eNewz kwamba anisameha kwa makosa yangu" alisema Barnaba
Hata hivyo Barnaba alisema siri ya mafanikio siyo kuvaa vizuri, kula vizuri au kuishi pazuri bali ni kuwa na heshima na kuepukana na malumbano na ugomvi usio wa lazima.

MSANII TID AFUNGUKA KUJA NA COLLABO NA DIAMOND PLATNUMZ

$
0
0
TID akiongea na  Clouds FM ambapo mkongwe wa muziki ambaye amepitia changamoto mbili tatu siku za hivi karibuni TID alikuwa akiachia ngoma yake mpya ambayo kamshirikisha FID Q inayoitwa Maisha ya Jela.

Ndipo alipoona kuwa sio mbaya kama akiwasanua wapenzi wote wa muziki mzuri kuwa siku za karibuni ataachia ngoma ambayo kamshirikisha Diamond Platnumz kwasababu ana ngoma ambayo anahisi Diamond Platnumz ndiye msanii ambaye atafit kwenye ngoma hiyo.
“Nina ngoma nafikiri itafaa zaidi nikimshirikisha Diamond. Diamond ameshapata habari nafikiri tutaifanya ngoma hiyo soon as possible” Alisema TID Mnyama.

MFAHAMU MISS TANGA 2001 ALIYEJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMA Mwanamke ukiamua kujitoa na kupigania nini unafanya lazima utafanikiwa, nami naweza kusema kufika kwangu ni pale nilipoamua kujituma, kujiamini na kutambua nini malengo yangu.
Hayo ni baadhi ya maneno aliyotoa mwanamke mjasiriamali Sophia Khalid Byanaku, ambaye ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Doctor's Plaza, alikuwa akizungumza na Globu hii. 
Sophia Khalid Byanaku ni mke wa Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), ana Elimu ya Shahada ya sosholojia (Degree in Sociology), Shahada ya uzamili Sera za afya Mipango na Usimamizi (Master in Health Policy Planning and Management.
Ulianzia wapi,

Byanaku : Mwaka 2001 nilishiriki mashindano ya urembo kwa mkoa wa Tanga na kufanikiwa kuchukua taji la Miss Tanga 2001 na kupata nafasi ya kuwa katika kumi bora ya Miss Tanzania ambapo taji lilichukuliwa na mrembo Millen Hapiness Magese. 
Unajivunia nn kupitia Miss Tanzania,
Byanaku: Najivunia mambo mengi kupitia ushiriki wa Miss Tanzania mwaka ule kwani umeweza kunipa ujasiri wa kuweza kupambana kwa namna nyingine na hata miaka yetu tuliweza kupata nafasi nyingi za kushiriki kijamii zaidi.
Baada ya kumalizika kwa Miss Tanzania ulijikita wapi zaidi:
Byanaku: Kabla ya kufungua Kliniki ya Doctor's Plaza, nilikuwa mfanyakazi wa benki Stanbic Bank Tanzania kwa takribani miaka 6, baadae nikafanya kazi benki ya NMB kwa muda wa mwaka mmoja na African Life Assurance (Sanlam).

Doctors Klinik ilianza lini?
Byanaku: Rasmi mwaka 2012 kwa kituo kimoja wakiwa wamejikita katika kutibu magonjwa ya moyo tu lakini sasa wanatoa matibabu ya ya magonjwa mbalimbali ya binaadamu na tayari wana vituo vitatu ambavyo vyote vipo jijini Dar es Saalam.
Madhumuni ya kufungua Doctors Kliniki ni nini?
Byanaku: Lengo kuu la kufungua vituo hivyo ni kwa sababu napenda sana kujishughulisha na jamii, hivyo kuwa na vituo hivyo amejua mambo mengi kuhusu jamii inayomzunguka. 
Matarajio ya Byanaku ya baadae:
Byanaku: Matarajio yangu ya baadae ni kuwa na Hospitali kubwa ya kisasa Tanzania ambayo itaweza kutoa huduma karibia zote kwa wahitaji,na pia nataka kuwa Mtaalam wa Health care Management kwa Tanzania,yani nataka kukiwa na uhitaji wa ushauri kuhusu masuala ya uongozi wa Afya Tanzania mimi niwe mtu wa kwanza kufikiria kusaidia.
Changamoto anazozipata katika vituo Doctor's Plaza
Byanaku: Kuna changamoto mbalimbali zinazotukabili kwenye vituo vyetu vya Doctor's Plaza ila kikubwa zaidi ni madaktari kwani ni wachache ambapo mpaka sasa tuna madaktari 32 kutoka Muhimbili ila tunaendelea kufanya jitihada kuhakikisha watu wanapata huduma wanazohitaji za matibabu. 

Anachojivunia kama mwanamke mjasiriamali:
Byanaku: Naweza kusema katika kufanikisha jambo uliloamua kulifanya, kwenye hili hakuna mwanaume wala mwanamke ili kuweza kufikia mafanikio yoyote,lazima kufanya kazi kwa bidii na kujituma,na sio kwa bidii tu lakini pia kwa akili,kusimamia malengo yako na pia kutokukubali kukatishwa tamaa na mtu yoyote yule,ilhali huvunji heshima ya mtu.
Wanawake tusiogope wala kuona aibu fursa zinapotokea tuzikimbilie bila aibu wala woga na tuonyeshe uwezo wetu, kwa kusema haya haya Mimi mwenyewe bado sijafikia malengo yangu lakini nashukuru nimeweza kufikia kidogo safari bado ni ndefu tunajifunza kila siku na nina amini nitafika.
Unapaswa kujiwekea malengo na kuyafanyia kazi ili kuyafikia, kila unachoona kinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa asilimia kubwa. 
Byanaku nje ya kazi ni nani?


Byanaku: Sophia Khalid Byanaku ni Mama wa watoto wawili, Nayla (6) na Akim(4), na nimeolewa na Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), muda wangu mwingi napokuwa nyumbani napenda kukaa na familia yangu.
Kama Mwanamke mara nyingi nakuwa na suluhisho na nafanikiwa kujigawa kwa usawa katika majukumu yangu ya nyumbani, napenda sana kuwa na familia pale ninapoukuwa nyumbani bila kuchanganya yote haya nayafanya na naweza ndiyo maana natarajia kuongeza zaidi hapa nilipoanza, kikubwa mwanamke unaweza kufanikiwa kama kweli umeamua kulifanya lako katika kuleta maendeleo katika jamii hasa iliyokuzunguka


Anasema hata hivyo bado anajitahidi kuwa nkujifunza kwa kusoma vitabu na hata kuuliza watu walionitangulia waliwezaje na kufanikiwa, lakini pia kuweza kufanikiwa haya ni lazima pia upate ushirikiano kutoka kwa familia,ambayo nashukuru ninapata ushirikiano.


Unapendelea nini? 


Byanaku: Ni mpenzi wa kusoma vitabu Sana kwa sasa nasoma vitabu viwili; My Personal MBA By Josh Kaufman na The E Myth Revisited By Michael Gerber na kitabu ninachotarajia kusoma ni The Miracle Morning by Hall Elroy. Napenda Kusafiri,Mziki,na kusoma.

MREMBO RAY C AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSU MSANII RAYVANNY

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Ray C amefunguka na kusema anamtamani sana msanii kutoka katika label ya WCB Wasafi Ray Vanny na amekuwa akipenda sana kazi zake na kuzisikiliza, hivyo anatamani kufanya naye kazi hata moja tu. 

Ray C alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema anasikia Ray Vanny anaandikia wasanii wengi sana nyimbo hivyo na yeye anatamani kufanya naye kazi kutokana na uwezo wake wa hali ya juu. 
"Nampenda sana yule mtoto Ray Vanny, anaadika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi" alisema Ray C 
Mbali na hilo Ray C alimzungumzia Diamond Platnumz kama msanii ambaye amefanya mapinduzi sana na kuupeleka muziki wetu wa bongo fleva mbali zaidi 
"Kiukweli mimi nam respect sana Diamond Platnumz amefanya jambo kubwa katika muziki wetu, kama hutaki kuelewa basi tu hutaki kuelewa, japo sisi tulikuwa tunasikika sijui Kenya wapi lakini dogo amepita sehemu zingine ambazo sisi hatukufika, ambaye haelewi mchango wa Diamond katika muziki huu sijui hata ana maana gani" alihoji Ray C  

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga Mutamba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

DKT MWAKYEMBE:MASOGANGE ALINILETEA NYODO

$
0
0

Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba ameendelea kufunguka changamoto zilizomkwamisha kudhibiti upitishwaji wa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati alipokuwa Waziri wa Uchukuzi hadi kuzidiwa kete na Agnes Masogange

Kupitia kipindi cha Breakfast cha East Africa Waziri Mwakyembe amesimulia kilichotokea wakati alipotaka kumdhibiti binti mmoja aliyedaiwa kupitisha masanduku matano ya ‘materials’ za kutengenezea dawa za kulevya aliyekamatwa nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania.

Amesema baada ya kufuatilia sakata lile mbali na kuchukua hatua kwa watu waliomsaidia kupitisha mzigo uwanja wa ndege, aliamua kufanya jitihada za kumkamata binti huyo ili achukuliwe hatua, lakini muda mfupi baada ya binti huyo kurejea nchini, yeye alihamishwa wizara, hivyo kukosa nguvu ya kumshughulikia, hatua iliyofanya binti huyo kumfanyia “nyodo”.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa binti ambaye alikamatwa nchini Afrika Kusini wakati huo kwa madai hayo, na kisha Waziri Mwakyembe kumfuatilia hadi kutimua baadhi ya watumishi wa uwanja huo Mwezi Agost mwaka 2013 alikuwa ni ‘video queen’ maarufu nchini, Agnes Geral d ‘Masogange’.

Aidha Mwakyembe amesema kijana wake mmoja anayefahamika kwa jina la Jingu ambaye yuko gerezani, anapaswa kuongezewa ulinzi kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa jemedari wa kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, lakini baadaye aliundiwa kesi na sasa huko gerezani anakutana na watu ambao wanaweza kumdhuru kutokana na kwamba yeye ndiye aliyesababisha wafungwe.

LE MAJANGAZ : MAMA AZAA WATOTO MAPACHA WAAJABU

STAA IRENE UWOYA AMPAMKANDA MZIMA WEMA SEPETU KUHUSU MASOGANGE

$
0
0

Lile sakata la masogange kuwekwa ndani kwa shutuma za madawa ya kulevya, limeingia ukurasa mpya baada ya hivi karibuni rafiki wa masogange ambaye pia ni staa wa filamu aitwaye Irene uwoya, kumjia juu wema sepetu baada ya kumtaja masogange kuwa mi miongoni mwa ma staa wanaotumia na kuuza madawa ya kulevya, staa hyo alitumia tafsida kufikisha ujumbe kwa wema sepetu kuwa alichokifanya sio ustaarabu ,alimtaka staa hyo kujifunza kutatua matatizo yake bila kumshirikisha mtu. 

Wema na uwoya ni mastaa ambao inasadikiwa wako kwenye bifu la chini kwa chini kwa muda mrefu, uenda sakata hili linaweza kuibua ugomvi mkubwa kwa mastaa hao wawili wenye mvuto wa aina yake

TOP 10 YA NCHI ZENYE WANAWAKE WAREMBO ZAIDI AFRICA

$
0
0
10: TANZANIA.
Wanawake wa nchi hii wanasifika kwa uzuri, kutunza nyumba na ujuzi kwenye kitanda. Kama unatafuta mwanamke wa kumpeleka nyumbani kumtambulisha ambaye anajua kutunza nyumba, Basi Tanzania ndipo eneo sahihi.


09: KENYA.
Wasichana wa Kenya niwazuri na wanamahaba, Kama unatafuta msichana ambaye ni mzuri, mwenye mahaba, na anaye jisimamia 'Independent', Mchapa kazi na sio mvivu... Basi kimbilia nchini Kenya.

08: GHANA.
Haitawezekana kukamilisha list ya nchi zenye warembo bila kupitia Gold Cost. Wanasifa ya kuwa Warefu, Wataalamu kitandani, ngozi ya asilia 'Ebony Skin tone' na wana uhalisi wa Muafrika.

07: NIGERIA.
Wanawake wa Nigeria niwazuri kutokana na ukubwa wa maziwa yao na walivyo jengeka miili yao kwa afya. Kati kati ya mwaka wa 1970s na 2011 nchi ya Nigeria imeongezeka kwa idadi ya watu nakusababisha iwe maarufu barani Afrika. Hivyo kama unataka mwanamke ambaye atakuzaliwa watoto wazuri basi Nigeria ndipo ukimbilie.


06: SOUTH AFRICA 'The famous Rainbow Nation'.
Afrika Mashariki ni nyumbani kwa wanawake warembo barani Afrika, kuwanzia Cape Town, Johannesburg, Pretoria na Durban. Wanawake wa Afrika Mashariki utawapata wenye uweupe wa chotara au uweusi halisi wa Afrika.
05: ANGOLA 'Doughters of Atlantic cost'.
Nchi ya Angola unaweza kusema ni kama Brazil ndogo kwa wasichana wazuri na warembo, Wasichana wake wakiwa wana rangi ya chocolate scados. Wasichana wa Angola baazi ni Supermodels ambayo itakuchanganya akili kabisa.
04: CAPE VERDE ISLAND.
Sio nchi maarufu barani Afrika wala hata kupata wataa kwenda kuitazama, Lakini kisiwa hicho kidogo ni nyumba ya wasichana na wanawake warembo walioumbwa Afrika. Wanakauli nzuri ya ukarimu ambayo itakufanya usahau njaa wakati hukula chakula.
03: ETHIOPIA 'The cradle of humanity'.
Ustaarabu ndipo ulipo anzia nchini Ethiopia, Wasichana wa nchi hii sio wazuri tu kwa bara la Afrika bali hata ulimwenguni wamekuwa wakisifika kwa uzuri wao unao shawishi kutangaza ndoa. Wengine wamekuwa wakidai uzuri wao umetokana na mchanganyiko wa mbegu 'uzazi' kutoka kwa watu wa Yeamen na Ethiopia wenyewe.
02: SOMALIA 'Vita haiondoi urembo'.
Kama hujawahi kukutana na msichana wa Kisomali basi utakapo kutana naye utachanganyikiwa na kukusababisha uweze hata kusaliti uliye naye. Chukulia mfano wa Iman, Model aliye tikisa ulimwengu kwa mwendo wake wa madaha hadi kila mmoja kushangaa. Wanasifika kuwa na macho mazuri, ngozi ya chocolate, nywele laini na ndefu.
01: RWANDA 'Africa's hidden Apple'.
Niwazuri na wakuvutia, Weusi wa asili, Wana umbo nzuri na ukarimu, Sauti ya kimahaba na urefu wakupagawisha. Wakitembea ni sawa na Twiga nyikani akiwa anatembea. Uzuri wao huwezi kuuelezea.

POLISI AFUNGUKA KWANINI DIAMOND PLATNUMZ HAKUFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0
Mohamed Mpinga ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania na amekubali kukaa kwenye Exclusive Interview na AyoTV kujibu baada ya watu ku-comment kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuona Diamond amepost picha akiwa na Kamanda na hakupelekwa Mahakamani.
Kamanda Mpinga ameeleza kwanini Mwimbaji Diamond Platnumz hakupelekwa Mahakamani baada ya video yake kusambaa akiendesha gari huku akiimba na kucheza wakati kuna wale wa Singida walipelekwa mpaka Mahakamani kwa kosa hilohilo.


THE TOP TEN MOSTLY DANGEROUS COUNTRIES IN THE WORLD

$
0
0
           1. SYRIA.

2. SOUTH SUDAN.
In the world there are many countries some have peace and some are very dangerous for the life of human being. There are some countries which are very dangerous for human being and every living organisms such as animals and the whole environments.

There are several factors considered to place the countries in the list of dangerous countries in the world such as civil war, robbery, religion misunderstanding. From these countries its impossible to invest because any thing can arise and take off the whole investment. Most of the dangerous countries in the world are coming from Africa and Asia countries.


3. IRAQ.





4. AFGHANISTAN.


5. SOMALIA.


6. YEMEN.


7. CENTRAL AFRICA.


8. PAKISTAN.


9. DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO.


10. SOUTH AFRICA. 

MREMBO MPYA ANAEKIMBIZA SASA HIVI HUKO KENYA,HUDDAH NA VERA CHALI

THE MAGAZETI YA BONGO LEO SATUDAY/JUMAMOSI 18/02/2017 LIVE

HUYU NDO MBUNGE MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI H.I.V …SASA KAFUKUZWA KANISANI

$
0
0
Aligunduliwa kuwa na virusi vya HIV mwaka 1997
Princes Kasune ni mmoja ya wanaharakati maarufu wa ugonjwa wa ukimwi nchini Zambia na alichaguliwa kama mbunge wa upinzani mwezi Agosti.Aligunduliwa kuwa na virusi vya HIV mwaka 1997 na mwaka uliofuatia alitangaza hadharani hali yake kinyume na mapenzi ya mmewe na tamaduni kwa kufanya hivyo.

“Wakati niligundua kuwa nilikuwa na virusi vya HIV, nilijua kuwa nilikuwa na jukumu la kueneza habari kuhusu njia HIV unaweza kuambukizwa, unaweza kuzuiwa na pia njia za kumaliza unyanyapaa,” Kasume mwenye umri wa miaka 40 aliiambia BBC.
Katika sehemu kubwa ya maisha yake, amethirika na virusi vya HIV. Alilelewa kijijini na aliwapoteza wazazi wake wote kwa ugonjwa wa ukimwi akiwa na umri wa miaka 14 na kisha akaolewa akiwa na umri wa miaka 18.
Anasema ana ana jukumu la kueneza habari kuhusu njia HIV unaweza kuambukizwa, unaweza kuzuiwa na pia njia za kumaliza unyanyapaa
Akiwa na ndoto na kuona kizazi kichajo kisicho na virusi vya ukimwi, uamuzi wake wa kutangaza hadharani hali yake ulizua tofauti kubwa.
Kanisa lake lilimtimua kwa kuchukua hatua hiyo na kwa kwenda kinyume na matakwa ya mmewe kuhusu kuweka siri hali yake ya kuishi na virusi vya ukimwi.
Amesafiri sehemu mbali mbali za dunia na kukutana na viongozi wakiwemo marais wa zamani nchini Marekani wakiwemo Bill Clinton na George W Bush pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Wakati mmoja akitoa hotuba, aliwakumbusha wabunge wenzake kuhusu umuhimu wa kupimwa hali zao.
Viewing all 23910 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>